SEHEMU YA KWANZA
Mtunzi ; Agatha Francis
“Kaka mbona unanikanyaga jamani,inamaana huoni kweli au makusudi tu”,ilikua sauti ya msichana akilalamika ndani ya dalala.”We dada vipi,kwani ulitakaje sasa,kazi kujilalamisha tu,usipotaka kukanyagwa ndani ya daladala nunua gari binafsi basi”,sauti ya kiume ilijibu,sauti ilijibu kwakujiamni sana kiasi kwamba kila mtu ndani ya gari alishangaa sana kiasi kwamba walithubutu kuingiliaa mabishano yale.Lakini kijana Yule wala hakujali mabishano yaliyoendelea ndani ya daladala,kituo kilichofuata yeye peke yake alishuka,watu wote walishangaa sana maana alikua kijana mdogo asiyekua na maadili hata kidogo,watu walimgeukia Evah kwakumpa pole nakumsihi amsamehe bure maana vijana waleo hawajui kuomba radhi wakoseapo.
Walipokua wakimpa pole Evah,konda aliyekua kimya kwa muda mrefu pia nae “akasema pole sana dada yangu msamehe tu,lakini mhhhhh alisita,kasha akasema nina wasiwasi na kijana Yule mbona miguu yake sijaelewa ni kama ina kwato sio kwato”,watu wote walishangaa kwaaaaatooo!!!!!!,tuyaache hayo itakua sijaona vizuri,konda alimaliza.Evah hakua nachakusema alibaki akijiwazia moyoni,sasa kwato kwangu mimi nimekosa nini?mmmh,namuachia Mungu wangu lakini mbona SINA KOSA lolote nililo fanya mimi.Aliachana na mawazo hayo kituo kilichofuata na yeye pia alishuka.
Alipokua akishuka alihisi maumivu kiasi mguuni,aliyapuuza kisha alitembea kwakuchechemea taratibu mpaka akafika nyumbani kwake.Akaingia ndani nakujitupa katika sofa lililokuwepo sebuleni kwake,alipoketi katika sofa hilo alianza kuona tofauti katika mguu wake,taratibu mguu wake ulianza kuvimba,Evah alianza kutawaliwa na hofu katika moyo wake.Kadri muda ulipokua ukisonga mbele mguu nao ulipamba moto hali ilizidi kumtisha Evah.Taratibu machozi yalianza kumdondoka,machozi yalizidi kumtoka kisha kilio cha sauti ya chini.Maskini mguu ule ulikua ukivimba uku ukiambatana na maumivu makali Evah alishindwa vumilia alianza kulia kilio cha sauti ya juu,kilio kile kilimshitua jirani yake aliyeishi chumba cha pili kutoka chumba chake,alikimbia haraka kuelekea chumbani kwa Evah.”Evah vipi tena jirani yangu mbona unalia kuna nini? Jirani aliuliza”E vah hakujibu alilia huku kidole chake kikionesha mguuni,Jirani alipiga magoti ili aone mguu unanini,”mmmmmh Evah umeufanya nini huu mguu tena jamani mbona unavimba na unaweka rangi nyeusi vidoleni”mimi pia nashangaa ndugu yangu,kuna mtu amenikanyaga kwa gari ndo imekua hivi,Evah alimaliza.Loooh!!!!!! huyo aliyekukanyaga sijui alivaa kiatu gani?Ngoja nichemshe maji nikukande,bila shaka hali itakua nzuri,jirani alisema.Basi jirani alianza kuyaandaa maji kwa ajili yakumkanda ndugu yake.Baada ya muda maji yalikua tayari alianza kumkanda jirani yake.Chakushangaza walichotegemea kilikua sicho,kila walipokua akimkanda hali ilizidi kua mbaya,mguu uliongezeka maumivu na ulivimba zaidi.Evah alilia kwa uchungu sana,jamani mguu wangu,nimekosa nini mimi?mbona maumivu makali kiasi hiki Mungu wangu.Alilia bila kupata majibu,Jirani sasa ndiye aliyepata kibarua chakumbembeleza jirani yake.Chukua simu mpigie wifi aje labda twende hospitali,Evah alisema hayo huku akiumia machozi yakimwagika usoni kama kamwagiwa maji,sura ya huzuni ndiyo iliyoonesha hayakua maji bali machozi.
Jirani alifanya kama alivyoagizwa na Evah,alichukua simu yake na kutafuta namba ya wifi kisha akaipiga.”Heloo,mimi jirani yake Evah naomba fanya upesi uje hapa anapoishi kwani anaumwa sana ili awahi hospitali”,jirani aliongea maneno yaliyojitosheleza,wifi hakua na lakusema zaidi alikata simu nakuanza kuelekea alipokua akiishi wifi yake,kwakua hawakuishi mali sana baada ya dakika kama ishirini tu wifi alikua amefika nyumbani kwa Evah.Alipofika pale alimkuta wifi yake amelala chini akilia kwa uchungu akisema mguu wangu,mguu wangu,wifi alipoutazama mguu maskini naye alishindwa jikaza akaanza kulia,Jirani akasema wifi huu si mda wa kulia katafute usafiri awahi kituo cha afya.Haraka jirani alijifuta machozi yake na kuanza kuelekea sehemu zinapopatikana tax.Alitembea kwa mwendo wa ajabu kiasi kwamba watu huko njiani walikua wakimshangaa maana hata miguuni hakuvaa viatu.Alifanikiwa kupata tax yaani gari kisha alirudi nyumbani kumchukua mgonjwa.Walifika hospitali haraka walionana na daktari,daktari aliukagua mguu kisha akasema,”dada yangu jikaze uvimbe wa kawaida tu,sasa hivi tutakuapatia tiba na mguu wako utakua sawa.Daktari hakujua maumivu aliyopata Evah hivyo wala hakusikilza aliendelea kulia lakini kwa wifi kidogo maneno ya daktari yalimtia moyo.Daktari alimuita muuguzi yaani nesi ili aanze kumtibia Evah,alimpa maelekezo yakufanya na dawa za kumpa baada yakumaliza kazi hiyo.Muuguzi aliitikia na kazi ikaanza.
*****
ITAENDELEA
1 Comments
safi sana simulizi nimeipenda sana
ReplyDelete